
Siku chache tu baada ya kuanza kurushwa hewani kwa kipindi
halisia cha televisheni(Reality Show) yake, muigizaji, mrembo maarufu nchini
Tanzania (Miss Tanzania 2006),Wema A. Sepetu, amepatwa na msiba mkubwa.
Amefiwa na Baba yake mzazi,Balozi Isaac Abrahamu Sepetu.
Taarifa ambazo BC imezipata zinapasha kwamba Mzee Sepetu
ambaye kwa muda wa miezi kadhaa sasa amekuwa akiugua na kusumbuliwa na maradhi
ya kiharusi,. Mzee Sepetu alikuwa pia akisumbuliwa na kisukari.Amefariki jijini
Dar-es-salaam. Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya
Sinza-Mori jijini Dar.
Wema katika picha ya pamoja na baba yake mzazi,Balozi Abraham Sepetu. Pembeni ni rafiki wa karibu wa Wema,Petitman
Pia, Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dr Mohammed Shein, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.
pole wema