Kiongozi huyo wa waasi alivuka na kuingia nchini
Uganda kwenye masururu wa magari mawili huku wanajeshi wa Umoja wa
Mataifa na wale wa DRC walipofika kilomita tano kuelekea katika kambi
yake ya kijeshi
Mwandishi wa BBC Ignatius Bahizi
amesema baada ya kuongea na afisaa mmoja wa usalama eneo la Bunagana
alimthibitisha kujisalimisha kwa Bisiimwa akisema kuwa anahojiwa na
maafisa wa usalama katika eneo la Bunagana katika mpaka wa Uganda na
Congo DRC.
Waasi wa M23 mnamo siku ya Jumatatu walitoroka
maeneo yao ya vita ikiwemo eneo la Rumangabo baada ya kukabiliwa na
mashambulizi kutoka kwa jeshi la UN na sasa inaarifiwa wametorokea
msituni.
Majeshi yanayopambana na waasi hao yamefanikiwa
kuwashinda waasi hao katika miji waliyokuwa wameiteka na sasa kuna
matumaini kuwa jeshi la DRC linaweza sasa kusitisha harakati za kundi
hilo ambazo zilianza miezi 20 iliyopita na ambazo zimewasababisha maelfu
ya watu kutoroka makwao wakikimbilia usalama wao.
Kundi hilo limekuwa kikiendeshea harakati zao katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa aliambia
baraza la usalama la umoja wa mataifa siku ya jumanne kuwa waasi wa M23
sio tisho tena na kuwa wameshindwa kijeshi baadhi wakikimbilia msituni
kutokana na mashambulizi makali kutoka kwa wanajeshi wa muungano
wanaokabiliana na waasi hao.
Naye msemaji wa UN nchini Uganda amesema kuwa
zaidi ya watu 5,000 wametoroka maeneo ya Bunagana kufutaia mapambano
makali kati ya waasi na wanajeshi wa DRC.
Lucy Beck wa shirika la kuwahudumia wakimbizi
alisema Jumatano kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka hadi 10,000 ifikapo
siku ya Alhamisi huku mapambano yakichacha katika mpaka wa Uganda na
Congo.
-BBC
-BBC
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.