Wednesday, October 30, 2013

PICHA ZA VIONGOZI WA SERIKALI NA WASANII MBALIMBALI WALIOJITOKEZA KUUGA MWILI WA MAREHEMU BABA YAKE WEMA SEPETU JANA

BABA mzazi wa staa wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu, Balozi Abraham Isaac Sepetu ameagwa jana jioni nyumbani kwake Sinza - Mori jijini Dar es Salaam.


Tukio hilo lilihudhuria na viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, Getrude Mongela pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe na wengine wengi waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia Jumapili ya wiki iliyopita.


Waziri Membe kwa niaba ya serikali ametoa salamu za rambirambi na kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1, “Kwa niaba ya serikali tumechangia kiasi cha shilingi milioni 1. Hata mimi pia nilimfahamu marehemu kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi makini, Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen,” alisema Waziri Membe.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa mazishi.





Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu enzi za uhai wake
Mh. Jaji Warioba  akisaini kitabu cha Maombolezo leo mchana nyumbani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akisaini kitabu cha maombolezo leo October 29, 2013 nyumbani kwa marehemu Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Mama Gertrude Mongella akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake Sinza Mori leo October 29, 2013


Mh. Jaji Warioba na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe wakibadilishana mawazo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo October 29,2013

Baadhi ya viongozi waliofika msibani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Watu wa karibu na marehemu waliokuwa wanaishi naye huko Zanzibar wakizungumza jambo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam
Mtoto mkubwa wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Aman Isaac Sepetu akizungumza jambo na mwandishi wa habari,  Mkwaia wa Kuhenga  leo October 29, 2013 nyumbani kwa Marehemu
Mtoto wa marehemu akimsalimia mama baada ya kufika msibani hapo leo mchana
Mama akiwa na mwanae baada ya kufika msibani
Wema Sepetu  (katikati) akiongea na Dada yake (wa kwanza Kushoto) na (kulia) ni mama yake mama yake mzazi
Kajala alishindwa kujizuia na kuanza kulia na kupelekea watu wengine kuanza kulia kwa majonzi
Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu ukifikishwa nyumbani kwake
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu likibebwa na kupelekwa ndani
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu likibebwa na kupelekwa ndani ya nyumba
Aman Isaac Sepetu ambaye ni mtoto mkubwa wa marehemu akitoka ndani na msalaba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu likitolewa ndani ya nyumba kwa ajili ya kufanyiwa maobi na kuagwa ili kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi
Wema Sepetu akiwa ameshikiliwa baada ya kuona mwili wa baba yake mzazi Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu ukiwa kwenye jeneza
Ilikuwa ni simanzi kubwa kwa Wema Sepetu
Wema Sepetu akiwa na simanzi nzito
Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu ukiwa ndani ya jeneza
Ndugu na jamaa wakiuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Ndugu na jamaa wakiuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Ndugu na jamaa wakiuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Ndugu na jamaa wakiuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Ndugu na jamaa wakiuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Ni simanza msibani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo leo October 29, 2013
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe akitoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Baadhi ya wanafamilia wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Mwendesha misa akitoa neno
Somo la mwenyezi mungu likisomwa wakati wa kuagwa kwa Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Mwili wa marehemu ukiombewa
Baadhi ya watoto wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Wasifu wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetua ukisomwa
Mtoto mkubwa na msemaji wa familia, Aman Isaac Sepetu akitoa shukrani kwa wale wote waliofika kuwafariji kwenye msiba wa baba yao mpendwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo October 29, 2013
Mke wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu akiwa na mmoja wa mtoto wa  Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Baadhi  ya ndugu na jamaa waliofika msibani

Ni majonzi






SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “PICHA ZA VIONGOZI WA SERIKALI NA WASANII MBALIMBALI WALIOJITOKEZA KUUGA MWILI WA MAREHEMU BABA YAKE WEMA SEPETU JANA ”

Post a Comment

 

FULL MAUDAKU Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter