Mwanamuziki na mwigizaji Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’,
amemshukia mwanamuziki memba mwenzake wa Candy n’ Candy, Top C na
kumtaka asimuingilie katika maisha yake.
Kupitia kipindi cha redio hivi karibuni, Top C alisema tangu Baby
Madaha asajiliwe katika kampuni hiyo ya muziki iliyopo nchini Kenya,
memba wengine wamekuwa wakipuuzwa na bosi wao, Joe Kairuki kiasi kwamba
hawasikiki kabisa na kuainisha kuwa Baby anatamba kwa sababu amekuwa
‘kiburudisho’ cha bosi huyo.
Alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, Baby alikanusha:
“Top C na wenzake ni wazushi, sina uhusiano na Joe. Mimi nina kipaji
kikubwa na nina nidhamu ya kazi kuliko wao ndiyo maana ninapewa nafasi.
Wanaendekeza uzushi kwa nini wasipigwe chini?”
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.