Wednesday, October 30, 2013

WANAJESHI WA KENYA WALIOPORA MALI KWENYE JENGO LA WESTGATE WAKATI WA SHAMBULIO LA AL-SHABAAB WATIMULIWA KAZINI..!!

Wanajeshi wawili nchini Kenya wamefutwa kazi na kufungwa jela baada ya kupatikana na kosa la uporaji wakati wa Oparesheni ya kukabiliana na wanamgambo wa Al Shabab katika jengo la Kibiashara la Westgate jijini Nairobi mwezi uliopita.


Picha za CCTV zikionesha wanajeshi wa Kenya wakiwa wamebeba mifuko ya plastiki


Mkuu wa Majeshi nchini humo Jenerali Julius Karangi amewaambia waandishi wa Habari kuwa mwanajeshi mwingine anachunguzwa na ikiwa atapatikana na kosa atafunguliwa mashtaka.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa jeshi amesisitiza kuwa ripoti ya vyombo vya Habari kuonesha kiwango kikubwa cha uporaji katika jengo hilo na wanajeshi si sahihi na hiyo ilikuwa ni mbinu ya wanahabari kuliharibia sifa jeshi la Kenya.

Kamera za CCTV ziliwaonesha wanajeshi hao baada ya Oparesheni wakiwa wamebeba  mifuko ya Plastiki wakiondoka ndani ya duka la jumla la Nakumatt na kuzua maswali mengi kutoka kwa wananchi wa nchi hiyo kutaka kujua walichokuwa wamekibeba ndani ya mifuko hiyo.

Angalia video tukio hilo hapo chini..


Awali, Jenerali Karangi alinukuliwa akikanusha madai ya wanajeshi kuhusika katika uporaji ndani ya jengo hilo na kusema kuwa walichokuwa wamekibeba wanajeshi yalikuwa ni maji ya kukata kiu baada ya kazi ngumu ya kupambana na magaidi hao.

Wamiliki wa maduka katika jengo hilo walijitokeza na kudai kuwa mali yao iliporwa na kupata hasara kubwa baada ya tukio la kigaidi lililoacha watu 67 kupoteza maisha.

Mapema wiki hii, jeshi la Polisi nchini humo lilisema kuwa linawashikilia washukiwa watano wanaohusishwa na shambulizi hilo ambao watafikishwa Mahakamani hivi karibuni na kufunguliwa mashtaka.

Wanamgambo wa Al Shabab walidai kutekeleza shambulizi hilo kwa kile walichokisema ni kwa sababu jeshi la Kenya limekataa kuondoka nchini mwao katika Oparesheni ya kuliangamizi iliyoanza mwaka 2011.

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “WANAJESHI WA KENYA WALIOPORA MALI KWENYE JENGO LA WESTGATE WAKATI WA SHAMBULIO LA AL-SHABAAB WATIMULIWA KAZINI..!!”

Post a Comment

 

FULL MAUDAKU Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter