Friday, November 08, 2013

AKATWA NYETI KWENYE MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI...

MBALI na mtu mmoja kufariki dunia na wengine 24 kujeruhiwa na kulazwa kwenye Hospitali ya Bwagala, Turiani mkoani hapa, mwanaume mmoja amekatwa nyeti zake katika mapigano ya wakulima na wafugaji Jumanne iliyopita.
Mapigano hayo yaliyoshuhudiwa na mwandishi wetu yalipoteza amani iliyokuwa  kwenye Kijiji cha Dihombo Kata ya Hembeti Wilaya ya Mvomero.
Mashuhuda kadhaa walimwambia mwandishi wetu kwamba, mtu aliyekatwa  nyeti alikutana na wakulima hao wenye hasira waliokuwa wakimvamia mgeni yeyote waliyemuona  mbele yao.
“Wakulima walikuwa na silaha za jadi kama vile mapanga, mishale ya sumu na marungu, walimkuta mtu huyo aliyekuwa akipita na kumvamia kisha kumpiga na alipoanguka chini mkulima mmoja alimkata nyeti zake,” alisema shuhuda aliyejitambilisha kwa jina la Kibwana.
Mtu aliyekatwa nyeti (angalia picha ukurasa wa mbele) hakufahamika jina lake mara moja, lakini baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kwamba alikimbizwa hospitali ili kunusuru maisha yake.
Hata hivyo, baadhi ya wakulima nao waliumizwa vibaya katika tukio hilo lililosababisha kifo cha mfugaji Yusuf Mdutu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa mapigano hayo huku akisema kuwa msako mkali unaendelea kuwakamata wahusika.

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “ AKATWA NYETI KWENYE MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI... ”

Post a Comment

 

FULL MAUDAKU Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter