Akizungumza kwenye kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Jokate alikiri kuwa mara nyingi alikuwa akijitahidi mno kukwepa maswali yanayohusu mahusiano yake hali iliyopelekea uhusiano wake na Hasheem usifahamike kwa watu wengi.
“Hashim Thabeet aka ‘Lulu’ nimedumu naye kwa miaka miwili mpaka mitatu na Diamond nimedumu naye kama siyo mwezi mmoja basi miwili,” alisema.
Jokate alisema baada ya hapo amekaa kwa kipindi cha mwaka mmoja mpaka sasa bila kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote hali iliyomfanya awe na uhuru wa kufanya mambo yake bila kusumbuliwa na mwanaume.
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.