Saturday, October 19, 2013


KATIKA hali ya kushangaza, staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja  amenaswa akiwa ametinga khanga moja na kuwaacha watu midomo wazi.
Kajala alinaswa na kamera yetu maeneo ya Kigogo jijini Dar ambapo watu kibao walionekana kumzunguka na kuhoji kulikoni staa huyo ambaye amezoeleka kutika pamba kali, aonekane na vazi la khanga?
Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Kajala alisema alilazimika kutinga khanga hiyo kuendana na matakwa ya filamu yaliyomtaka kuvaa vazi hilo na kuonesha mazingira ya uswahilini hivyo watu waliomzunguka walikuwa hawajui nini kinaendelea.
Nilipoambia naigiza sinema ya Kigodoro nilishtuka sana lakini mwisho wa siku nilikubali kwa kuwa mimi ni msanii naweza kubadilika kivyovyote na nina imani mashabiki wangu wataniona kivingine, humo ni full mcharuko,” alisema Kajala.

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “ ”

Post a Comment

 

FULL MAUDAKU Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter