STAA wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema anainjoi kuishi maisha ya ubachela hivyo haoni umuhimu wa kuoa.
Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akitema mbili tatu mbele ya kinasa sauti cha Stori, Ray aliyetamba
kwenye sinema ya Ramadhani, alisema kwenye maisha yake anapenda zaidi
kuwa bachela tofauti na wasanii wenzake ambao ndoa wanaona ni kitu cha
haraka na kukipa kipaumbele.
“Napenda maisha haya, sina mpango wa kuoa kwa sasa, niko
kivyanguvyangu na suala la kuoa kwangu bado ni kitendawili ambacho bado
sijakipatia majibu,” alisema Ray au The Greatest.
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.