Sunday, October 20, 2013

NISHA: MUZIKI NILIFUATA MKUMBO, NAJUTA

STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kujihusisha na masuala ya muziki, isipokuwa aliingia katika fani hiyo kwa kufuata mkumbo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nisha  alisema imekuwa ni aibu kubwa kujikita kwenye fani hiyo na kukaa kimya kwa kipindi kirefu kwa kuwa hana mapenzi ya dhati na fani hiyo kama ilivyo kwenye filamu.

“Niliona waigizaji wanaingia kuimba na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana  najuta, nimeamua nikae chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu,” alisema Nisha.

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “NISHA: MUZIKI NILIFUATA MKUMBO, NAJUTA”

Post a Comment

 

FULL MAUDAKU Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter