![]() |
Mke wa marehemu, Leah Nyaisangah akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe. |
![]() |
Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani kwa marehemu Julius Nyaisangah eneo la Kihonda Mtaa wa Viwandani mkoani Morogoro. |
MAREHEMU Julius Nyaisangah 'Uncle J' amefariki dunia leo asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu. Akizungumza na Mtandao huu, Mke wa marehemu, Leah Nyaisangah amesema kuwa mumewe alilkuwa akisumbuliwa na magonjwa ya sukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu na amefariki leo asubuhi. Marehemu Nyaisangah mpaka mauti yanamfika alikuwa Meneja Mkuu wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro. Marehemu ameacha mke na watoto watatu ambao ni Samwel, Noela na Beatrice. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika nyumbani kwao Tarime.
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.