Msanii wa label ya Candy n Candy Baby Joseph Madaha amekanusha uvumi uliovumishwa na wanamuziki wenzake wa labe hiyo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na CEO, Joe Kariuki.
Uvumi huo ulianzishwa na baadhi ya wasanii wengine, wa label hiyo
wanaodai kuwa tangu Baby Madaha asainishwe Candy n Candy maisha yake
yamebadilika na kwamba amekuwa akipendelewa zaidi.
Akizungumza Bongo5 jana , Baby amesema CEO wa Candy N Candy, Joe
Kariuki alishauriwa na wadau kwamba amwendeleze yeye na akifanikiwa
awasaidie na wenzake.
“Joe amesikia na hajapenda hili swala kwasababu sisi tupo kizazi
zaidi kwasababu mimi najituma kufanya kazi ya muziki ambayo imenipeleka
Candy n Candy na sio mambo mengine kama wanayosema wao.
"Huu ni wivu ni
kwasababu mimi ni msanii mkubwa tayari nimeshatengeneza jina kwenye
muziki sema kuna kipindi nilijikita kwenye filamu sana, kwahiyo siwezi
lingana nao hata kidogo,” amesema.
“Candy n Candy walihitaji mwanadada ambaye ataweza kuongea zaidi ya
lugha mmoja kwasasababu ya kufanya muziki kimataifa na kigezo kingine
walichokitaka ni huyo mwanamuziki mwanadada kuwa na mwenekano mzuri.
" Wasanii wote wa Candy n Candy tulipelekwa studio, tukarekodi kila
msanii.Wale Four – D ndio walianza kurekodi sasa kukawa na msichana
mmoja anatoka kimapenzi na msanii mwezake wakawa wanatukanana na
kushikanashikana pamoja na kumsema bosi wao.
"Baada ya kurekodi bosi
akapokea ushauri kutoka kwa wadau kwamba ‘hii kazi ya Four – D ni mbaya
kwanini usimwendeleze Baby Madaha halafu baadaye Baby Madaha akawainua
wenzake’.
"Bosi akatuambia ‘sasa ngoja nianze na Baby Madaha nyie wengine mtafuata’ wale Four – D hawakuwa wavumilivu ndio wakaanza kusema maneno mengi,” amefafanua Baby na kuongeza
“Kiukweli mimi najituma katika kazi, Top C wanataka wafanyiwe kila
kitu watafutiwe kila kitu.
"Kwahiyo mimi naona kama wangenisikiliza mimi
kama mimi kwasababu nimepitia kwenye academy ya muziki kwahiyo naulewa
muziki, haikuwa na sababu ya kuongeaongea maneno mtaani.
"Mpaka leo Top C
anapigiwa simu akafanye video hawajaenda wanasema ana matatizo ya
kifamilia, sasa ni bosi gani aache kufanya kazi na watu ambao wako
serious amfuate yule aliye bize?"
Hata hivyo Baby amesema kwa kuwa Joe ni mwanaume na yeye ni mwanamke
endapo wakiwa wapenzi si japo la kushangaza wakikubaliana kufanya hivyo.
“Haya ni mafanikio yangu ndio maana wanaongea,leo nimezindua bag na
perfumes wana wivu, kwani Joe si yupo single na mimi nipo hivyo hivyo!!
Kwahiyo kama tukikubalina personal ni sisi,muziki ni muziki na mapenzi
ni mapenzi. Kwahiyo yote yanawezekana.”
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.