Thursday, November 07, 2013

DEREVA ACHEZEA KICHAPO KWA KUMGONGA MTOTO MWANANYAMALA JIJINI DAR...!! TAZAMA PICHA ZA TUKIO ZIMA HAPA..




Dereva mwenye tisheti nyekundu akipokea kichapo kutoka kwa wananchi baada ya kumgonga mtoto na kutaka kukimbia eneo la Mwananyamala jijini Dar.
Dereva akiwa hoi kwa kipigo.
Wananchi wakiwa wamelizingira daladala lililogonga mtoto wakati wengine wakiendelea kumshushia kichapo ndani ya gari.

JANA ilikuwa siku mbaya kwa dereva wa daladala lenye namba za usajili T 782 BCR linalofanya safari zake Mabibo, Mwananyamala / Makumbusho baada ya kumgonga mtoto eneo la Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Baada ya tukio hilo, dereva alijaribu kukimbia kutoka eneo la tukio lakini alidakwa na wananchi na kupewa kichapo cha haja. 

Baada ya kipondo kutoka kwa wananchi hao waliokuwa na hasira, dereva huyo alipelekwa polisi ambapo mtoto aliyegongwa alikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala kupata matibabu.

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “DEREVA ACHEZEA KICHAPO KWA KUMGONGA MTOTO MWANANYAMALA JIJINI DAR...!! TAZAMA PICHA ZA TUKIO ZIMA HAPA.. ”

Post a Comment

 

FULL MAUDAKU Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter