
Serikali imesema licha ya kutokea mvutano kati yake na nchi za Rwanda, Kenya na Uganda, hadi sasa haijafikia dhamira ya kujitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba mgogoro uliopo utamalizwa kidiplomasia kwa lengo la kudumisha uhusiano uliopo.
Leo bungeni Dodoma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema lengo la Tanzania ambayo ni walengwa wakubwa ni kuona muungano huo unakuwa wenye tija kwa wananchi wa nchi wanachama na si kwa upande mmoja tu
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.