Habari Admin,
Naombeni
msaada wa maawazo yenu, nimegundua kuna mwanamke anatembea na mume
wangu, mume wangu alikataaaaaa kwa mara ya kwanza, lakini baada ya
kufatilllia na kuchunguza kwa muda mrefu nikaja kuhakikisha ni kweli
kabisa, mwanamke anaomba msamaha kwamba wataachana na hatorudia tenaa,
na mume wangu pia anasema hatorudiaa,
Nimeumia
sana mwenzenu, nimeumia kupita kias, kwakuwa nilimpenda, nilimheshimu,
nilimjali sana mume wangu, nilikuwa teyari kumuachia yeye kila kilicho
changu, nilimsikiliza sana, sikutegemea kama atakuja kunitenda hivi,
imekia kipindi najuta kwanini niliolewa nay eye, sikutegemea
kabisa kutokana na muonekano alio nao,,, details zoote za huyo mwanamke
wake niko nazo, niliomba niprintiwe kupitia mitandao ya simu
wanayotumia, niko nazo mkononi, staki kuamini, ninalia kama mtoto mdogo,
ni bora niibiwe pesa nitatafuta, kuliko kuibiwa penzi,, nitalipata
wapi,,
Nimechanganyikiwa,
nataka kuondoka kwenda kwetu nikapumzike, nimwache kwanza, maana kila
nikimuona Napata hasira natamani kumkaba kabisa, nimemchukia mno,,, sina
amani ya kuwa nay eye, hali hii hadi lini?? Nifanyaje?
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.