Baba
mzazi wa mabinti wawili mkazi wa Kijiji cha Kiria Kata ya Mamba Kusini,
wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, amewabaka na kuwalawiti binti zake
hao wenye umri wa miaka 10 na 13 na kuwajeruhi vibaya.
Kitendo
cha baba huyo kufanya unyama huo kimedaiwa kuwapandisha hasira kinamama
wa kijiji hicho walioamua kumkamata na kumpeleka Kituo cha Polisi Himo
huku wakitishia kumuua iwapo polisi watamwachia huru, kwa madai imekuwa
ni kawaida yao kila akifikishwa kituoni hapo kuhusiana na unyama
anaowafanyia watoto hao huachiwa.
Mwanamume
huyo anadaiwa kuwa na tabia ya kuwatendea vitendo hivyo wanaye hao kwa
muda mrefu, kutokana na ugomvi baina yake na mkewe uliosababisha mkewe
akimbie na kuwaacha watoto hao na baba huyo.
Akizungumza
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiria, Doroth Mtui, alisema taarifa hizo
alizipata kutoka kwa majirani wa watoto hao, ambapo mtoto mmojawapo
alimweleza kwa undani juu ya ukatili huo na baadaye walimkamata
mwanamume huyo na kumpeleka Kituo cha Polisi Himo.
Alisema walipofika kituoni, walitakiwa kumpeleka mtoto huyo hospitalini ili kuthibitisha kama kweli amebakwa.
Taarifa
iliyotolewa na daktari wa Hospitali Teule ya Kilema, ilionyesha mtoto
huyo kuharibiwa sehemu zote mbili na kwamba kitendo hicho kimekuwa
kikifanyika kwa muda mrefu.
Mtui
alidai kuwa mwanamume huyo, alikuwa akiishi na watoto hao wawili ambao
aliwatumia wote kwa zamu na kwamba mtoto mdogo, alifanikiwa kutoroka na
mpaka sasa hajulikani aliko, aliendelea kumtendea ukatili huo mtoto
aliyebaki huku akimtisha kumuua iwapo atatoa siri hiyo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema polisi wamekamilisha uchunguzi na huenda mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani wakati wowote.
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.