Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kapteni Mstaafu, John Komba amevunja ukimya na kutamka wazi kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ndiye chaguo lake na atakuwa Rais ajaye uchaguzi wa 2015.
Komba anakuwa mtu wa pili kumtaja Lowassa hadharani kuwa anafaa kuwa rais 2015.
Itakumbukwa
Mbunge wa Viti Maalumu, Beatrice Shelukindo (CCM) naye alivunja ukimya
baada ya kutangaza kumuunga mkono Lowassa kumrithi Rais Kikwete.
Shelukindo
alitoa kauli hiyo wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya
kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT, kwenye sherehe za
kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa na kuhudhuriwa
na makada kadhaa wa CCM.
Akizungumza
na Mwananchi katika mahojiano maalumu jana, Komba ambaye ni Kiongozi wa
Kundi la Uhamasishaji cha CCM Tanzania One Theatre (TOT Plus), alisema
mtazamo wake kwa mtu anayefaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete ni Lowassa.
Komba
aliyeingia kwenye siasa kutokana na msukumo wa mama yake aliyekuwa
msaidizi wa Bibi Titi Mohamed, alisema anazo sababu kuu tano za
kumkubali Lowassa kuwa Rais na atasimama popote kumtetea.
“Nakuambia Lowassa ndo anafaa kuwa Rais na nina sababu zangu tano za kusema hivyo,” alisema Komba na kuhoji:
“Wewe
unakwenda kwenye harambee, nani leo hii anaweza kusaidia kuchangia
fedha nyingi na zote hizo ni kwa maendeleo yanayokusudiwa kama siyo
Lowassa?” alisema Komba ambaye ni mahiri katika kuinadi CCM, katika
kampeni mbalimbali za udiwani, ubunge na urais.
Juu ya kuwa atakuwa katika wakati mgumu endapo anayempigia debe hatokuwa Lowassa, Komba alisema:
Juu ya kuwa atakuwa katika wakati mgumu endapo anayempigia debe hatokuwa Lowassa, Komba alisema:
“Mimi
nimesema namkubali Lowassa, lakini kama akiteuliwa mwingine, mimi
nitakuwa naye...nitamwimbia hadi mwisho. Kazi yangu si unaijua,
nitampigia debe kwa kuwa si mtu wa mtu mmoja, ni uteuzi wa wanaCCM ule
si wa Komba.” .
Mbali
na kumnadi Lowassa, Komba alisifu uimara wa chama chake kuwa
kinaimarika siku hadi siku na ndicho kinachotoa viongozi wa kweli na
hata wananchi wanakikubali.
Akizungumzia
suala la rushwa ndani ya CCM, Komba ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga,
alisema kama chama kuna watu wa aina nyingi, kuna wasafi, kuna wachafu
lakini wote wako kwenye mstari mmoja.
Alisema kuwa vita ya rushwa ndani ya CCM itamalizika endapo kila kiongozi atasimamia haki na maadili ya uongozi na pia kutambua wajibu wake ndani ya chama.
-Mwananchi
Alisema kuwa vita ya rushwa ndani ya CCM itamalizika endapo kila kiongozi atasimamia haki na maadili ya uongozi na pia kutambua wajibu wake ndani ya chama.
-Mwananchi
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.